Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Ni chombo huru kilichoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (Sura ya 79). Jukumu lake kuu ni kusuluhisha migogoro inayohusiana na masoko ya mitaji, kuhakikisha kwamba kila mshiriki katika sekta hii wakiwemo wawekezaji, mawakala, washauri wa kifedha, kampuni zilizoorodheshwa na...
Ni chombo huru cha kisheria kinacholenga kukuza usawa na imani katika masoko ya mitaji ya Tanzania. Baraza linasimamia usuluhishi wa migogoro kati ya wawekezaji, mawakala wa masoko, kampuni zilizoorodheshwa, na wadhibiti, pamoja na kupokea na kushughulikia rufaa dhidi ya maamuzi yaliyotolewa na Maml...
Hapana. Baraza ni chombo cha kisheria cha haki madai (quasi-judicial) kinachoshughulika na usuluhishi wa migogoro na rufaa zinazohusiana na masoko ya mitaji.
Kwa upande mwingine; DSE (Soko la Hisa la Dar es Salaam) ni soko la wazi ambapo dhamana kama his ana hati fungani hununuliwa na kuuzwa; UTT...
Rufaa kwa Baraza hutoka kwa watu binafsi au taasisi ambazo hazijaridhika na maamuzi yaliyotolewa na Mamlaka ya Usimamizi au watu na zilizo kwenye migogoro ndani ya masoko ya mitaji.
Masuala ya leseni (kama vile kukataliwa kwa leseni, kusitishwa au kufutwa);
Migogoro inayohusu dhamana (ikiwa ni pamoja na kukataliwa kuorodheshwa, kusimamishwa kwa biashara au kuondolewa sokoni);
Migongano kati ya washiriki wa soko (kwa mfano kati ya mawakala wa soko na wateja, au kati ya kam...
Ndiyo. Maamuzi yanayotolewa na Baraza la Masoko ya Mitaji (CMT) yanaweza kukatiwa rufaa kwenda Mahakama ya Rufani Tanzania lakini kwa hoja za kisheria pekee si kwa masuala ya uthabiti wa kesi.
Anapaswa kuwasilisha taarifa ya notisi ya nia ya kukata rufaa ndani ya siku 7 tangu kutolewa kwa uamuzi wa Mamlaka unaopingwa.
Anatakiwa kuwasilisha taarifa ya hati ya rufaa pamoja na nyaraka zinazohusu rufaa hiyo ndani ya siku 30 kutoka tarehe ya uamuzi unaopingwa.
Ndiyo. Baada ya Baraza la Masoko ya Mitaji kutoa maamuzi, yanaweza kubadilishwa kuwa amri rasmi, iliyotiwa saini na Mwenyekiti au Msajili, na kutekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai (Sura ya 33).
Baraza lina mamlaka ya kutoa adhabu au suluhu kwa migogoro iliyowasilishwa, kuruhusu hatua za utekelezaji wa kisheria au kuhakikisha utekelezaji na utii wa maamuzi yake.
Iwapo mtu atakataa kutekeleza maamuzi ya Baraza la Masoko ya Mitaji, Baraza lina uwezo wa kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha kuwa maamuzi hayo yanatekelezwa ipasavyo, sawa na jinsi mahakama ya kawaida inavyofanya.