Je, mtu anapaswa kufanya nini ili aweze kukata rufaa kwa Baraza la Masoko ya Mitaji?
Anapaswa kuwasilisha taarifa ya notisi ya nia ya kukata rufaa ndani ya siku 7 tangu kutolewa kwa uamuzi wa Mamlaka unaopingwa.
Anatakiwa kuwasilisha taarifa ya hati ya rufaa pamoja na nyaraka zinazohusu rufaa hiyo ndani ya siku 30 kutoka tarehe ya uamuzi unaopingwa.