+255738785651 info@cmt.go.tz

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA FEDHA

BARAZA LA MASOKO YA MITAJI

CMT Logo
NYARAKA ZA RUFAA

Uwasilishaji wa rufaa

  1. Utaratibu wa kukata rufaa kwa Baraza utaanza kwa kuwasilisha Maelezo ya Rufaa kwa Msajili wa Baraza ndani ya siku thelathini (30) tangu tarehe ya uamuzi wa Mamlaka unaokatiwa rufaa.
  2. Maelezo ya Rufaa yataandaliwa kwa kutumia Fomu Na. 2 ya CMT, kama ilivyoelekezwa kwenye Jedwali la Tatu kwenye Kanuni.
  3. Kila rufaa itapaswa kujumuisha viambatanisho vyote muhimu vitakavyofanikisha kushughulikiwa kwa rufaa.

Nyaraka Muhimu

4. Bila kuathiri Kanuni Ndogo ya 2, rufaa itapaswa kuambatanishwa na nyaraka zifuatazo;

        a)Nakala iliyoidhinishwa ya uamuzi wa Mamlaka

        b) Nakala iliyoidhinishwa ya mwenendo wa shauri lililoendeshwa na Mamlaka

        c) Nakala ya Tangazo la Nia ya Kukata Rufaa

       d)Maelezo ya Rufaa

     e) Nyaraka nyingine zozote mleta maombi atakazoona zina umuhimu katika kuhakikisha rufaa inasikilizwa       kikamilifu bila upendeleo.

5. Katika kuzingatia Kanuni Ndogo ya 4(b), “mwenendo” si lazima ujumuishe vielelezo na viambatanishi vilivyowasilishwa wakati wa usikilizaji wa shauri kwenye ngazi ya Mamlaka.

6. Baraza linaweza, kwa utashi wake, kuhitaji kuwasilishwa kwa vielelezo na viambatanishi vilivyoletwa wakati wa usikilizaji wa shauri na Mamlaka.