Baraza likiwa kama taasisi inayojitegemea kwa ajili kusikiliza rufaa zinazotokana na migogoro kati ya washiriki wa masoko, wawekezaji, na Mamlaka katika masuala yote ya masoko ya mitaji na dhamana
Baraza ikiwa ni taasisi inayojitegemea, lina jukumu la kusimamia utekelezaji wa sheria za masoko kwa kutoa adhabu kwa wadau ambao wamevunja taratibu za masoko kupitia maamuzi ya Baraza. Baraza lina mamlaka kamili ya Mahakama Kuu katika utekelezaji wa majukumu yake
Baraza lina Mamlaka ya kupitia maamuzi yaliyotolewa na Mamlaka kuhusiana na masoko ya mitaji kwa lengo la kuhakikisha maamuzi hayo yanazingatia sheria na hayapo kinyume na haki za washikiri wa masoko