Dira na Dhamira
Dhima
Kuwa Baraza inayoongoza katika Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa ajili ya uamuzi wa rufaa zinazohusiana na masoko ya dhamana kwa haki na uwazi, ikichochea imani ya wawekezaji na kudumisha uadilifu wa kifedha.
Dhamira
Kuhakikisha utatuzi wa haki, usawa, na kwa wakati wa migogoro na tofauti kati ya washiriki wa masoko ya dhamana.
Maadili ya Msingi
- Mwelekeo kwa Wateja
Wakati wote, Baraza inaweka wateja kwanza kwa kutoa huduma bora. - Utaalamu
Baraza inazingatia maadili yaliyowekwa ambayo yanajumuisha wajibu wa kitaaluma, kanuni za mwenendo, na matarajio rasmi na yasiyo rasmi ya wateja katika utoaji wa huduma zetu. - Ubunifu
Baraza inawaza kila mara jinsi ya kuboresha na kuongeza thamani ya ziada kwa kufanya mambo tofauti, kila wakati ikitafuta njia za kufanya mambo kuwa bora na kufanya kazi na mawazo mapya.. - Uadilifu
Baraza inaongozwa na kanuni za kimaadili, uaminifu, na uadilifu katika mahusiano yetu yote ya kazi na maamuzi. - Ufanisi
Kuongeza uwezo wa kutekeleza majukumu kwa kutumia rasilimali kidogo iwezekanavyo. - Usimamizi Shirikishi
Kujaribu kuwahimiza wafanyakazi kushiriki katika mchakato wa kufanya maamuzi ya Baraza.