+255738785651 info@cmt.go.tz

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA FEDHA

BARAZA LA MASOKO YA MITAJI

CMT Logo
Majukumu Yake

Baraza la Masoko ya Mitaji (CMT) la Tanzania ni chombo maalumu na huru cha maamuzi kilichoundwa kuhakikisha kunakuwepo usawa, uwazi na ulinzi kwa wawekezaji ndani ya mfumo wa masoko ya mitaji. Majukumu yake ya msingi yana mamlaka ya kimahakama na kiusimamizi, yakizingatia uhalisia wa masoko ya kifedha unaobadilika mara kwa mara kutokana na mazingira ya sekta yenyewe.

 

Majukumu ya Msingi ya Baraza la Masoko ya Mitaji

  1. Utatuzi wa Migogoro   

Baraza linatolea maamuzi migogoro inayojitokeza chini ya Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana [Sura ya 79], ikiwemo;

  • Migogoro baina ya Mamlaka na masoko ya hisa au madalali wa masoko
  • Migogoro baina ya madalali na wateja wao
  • Mivutano inayohusisha kampuni zilizopo kwenye masoko ya hisa, mamlaka za usimamizi, au masoko ya dhamana
  • Rufaa dhidi ya maamuzi yahusuyo leseni, kusitishwa kwa uuzaji wa hisa, au kuorodheshwa kwa dhamana

 

  2. Kutafsiri Sheria

Baraza hutafsiri sheria na kanuni zinazohusu masoko ya mitaji, likitoa ufafanuzi wa kimamlaka juu ya vifungu vinavyosimamia uendeshaji wa masoko hayo.

  3. Mfumo wa Rufaa

Baraza ndiyo jukwaa la msingi la maamuzi kwa pande zisidhoridhishwa na maamuzi ya Mamlaka. Linatoa utaratibu wenye mpangilio:

  • Kuwasilisha Tangazo la Nia ya Kukata Rufaa ndani ya siku saba (7) tangu uamuzi ufanyike
  • Kuwasilisha Maelezo ya Rufaa yaliyokamilika ndani ya siku thelathini (30) tangu uamuzi ufanyike.

 

  4. Ulinzi kwa Wawekezaji

Kupitia utatuzi wa migogoro wenye ufanisi na uwazi, Baraza linalinda haki za wawekezaji na kukuza imani kwenye masoko ya fedha ya Tanzania.

 

  5. Mamlaka ya Kimahakama

  • Baraza lina mamlaka sawa na Mahakama Kuu, ikiwemo;
  • Kuita mashahidi
  • Kuapisha
  • Kuamuru upatikanaji wa nyaraka
  • Kutoa maamuzi ya mwisho kwenye masuala ya msingi (yanayoweza kukatiwa rufaa kwa kufuata vifungu husika vya sheria tu).

Nafasi ya Kimkakati katika Uadilifu kwenye Masoko

Baraza lina umuhimu kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo (Dira 2050), likichangia katika;

  • Utawala bora
  • Ufafanuzi wa sheria
  • Ukuaji endelevu wa kiuchumi
  • Uongozi kikanda kwenye utoaji wa maamuzi kwenye masuala ya masoko ya dhamana