Utoaji wa Miongozo
Baraza la Masoko ya Mitaji ni maalumu kwa ajili ya kukuza uelewa, uwazi na utambuzi wa taratibu za kimfumo kwenye masoko ya mitaji nchini. Kupitia jukumu lake la kutoa muongozo, Baraza linawezesha uwepo wa muelekeo wa kimamlaka kwenye masuala ya kisheria na usimamizi yanayohusu washirika wa masoko, wawekezaji na taasisi.
Tunatoa muongo kwa:
- Kutafsiri vifungu vya Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana [Sura ya 79] na kanuni zake
- Kufafanua matakwa ya taratibu za rufaa na usuluhishaji wa migogoro
- Kuelezea kwa kina jinsi ya kuzingatia matakwa ya kiutaratibu na uendeshaji wa shughuli za masoko ya mitaji
- Kutoa ufafanuzi kwa wadau pale wanapohitaji uelewa zaidi juu ya taratibu za Baraza
Utoaji wetu wa miongozo unasaidia mfumo wa kisheria kueleweka, kupunguza wasiwasi na kuwawezesha wadau kushiriki kikamilifu kwenye masoko ya mitaji nchini. Iwe unaandaa rufaa, unatafuta leseni au unahitaji uelewa juu ya usimamizi wetu wa sheria, Baraza liko maalumu kwa ajili ya kuwezesha maamuzi sahihi na kuhakikisha kanuni za usawa na urahisi katika shughuli za masoko ya mitaji zinafuatwa.