JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA FEDHA

BARAZA LA MASOKO YA MITAJI

Karibu

Karibu kwenye Tovuti Rasmi ya Baraza la Masoko ya Mitaji (CMT)

Baraza la Masoko ya Mitaji ni taasisi ya kisheria iliyoanzishwa chini ya Kifungu cha 136A cha Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana [SURA 79 Toleo la 2002] kama ilivyorekebishwa mwaka 2010 (inayorejelewa hapa kama Sheria). Mamlaka ya Baraza yanatolewa chini ya Kifungu cha 136G cha Sheria kama ifuatavyo, "Baraza litakuwa na mamlaka ya kutoa maamuzi juu ya migogoro na utata unaotokana na Sheria hii." Katika utekelezaji wa majukumu yake, Baraza linaongozwa na Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025, Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDPIII) 2021/22- 2025/26, Ilani ya Chama cha Mapinduzi - 2020 na Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Ahsante.