Utekelezaji wa kanuni
Baraza la Masoko ya Mitaji lina jukumu la muhimu katika kusimamia uadilifu kwenye masoko ya mitaji nchini kwa kuhakikisha kuwa maamuzi ya mamlaka za usimamizi yanatekelezwa kwa usawa, uwazi na kwa kufuata sheria.
Mamlaka inapotoa adhabu, mazuio au kufuta leseni, pande zilizoathirika zina haki ya kupinga maamuzi hayo mbele ya Baraza. Kupitia jukumu lake la kuhakikisha sheria na kanuni zinafuatwa, Baraza
- Hupitia uhalali kisheria na usawa wa hatua za kiusimamizi zilizochukuliwa na Mamlaka
- Huamua endapo adhabu, usitishaji au uzuiaji uliowekwa kwa washiriki wa masoko na Mamlaka umefuata sheria
- Huhakikisha kuwa utekelezaji wa maamuzi umezingatia kanuni za zinazotaka utaratibu ufuatwe na wawekezaji walindwe
Baraza linaweza kuthibitisha, kutokukubali au kutengua utekelezaji wa maamuzi, na pale inapobidi, kutibu mapungufu ili kuhakikisha taratibu zainafuatwa na hivyo kurejesha imani kwenye masoko. Maamuzi yake yana nguvu ya kisheria, hivyo kuchangia kujenga mazingira ya kifedha yaliyo imara na yanayoaminika.
Kwa kuhakikisha kunakuwepo mfumo wa utatuzi wa migogoro wenye taratibu mahususi, Baraza linaimarisha uwajibikaji katika usimamizi na kuhimiza nia ya taifa ya kuwa na mfumo wa masoko ya mitaji wenye usawa, ulio jumuishi na wenye uwazi.