+255738785651 info@cmt.go.tz

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA FEDHA

BARAZA LA MASOKO YA MITAJI

CMT Logo
Utatuzi wa Migogoro

Kwenye Baraza la Masoko ya Mitaji tunatoa jukwaa lenye uswa, ufanisi, na uhuru kwa ajili ya utatuzi wa migogoro inayojitokeza kwenye mfumo wa masoko ya mitaji nchini. Iwe ni mwekezaji, dalali, kampuni iliyoorodheshwa kwenye soko la hisa, au mamlaka ya usimamizi, jukumu letu ni kuhakikisha haki inapatikana kwa uwazi, haraka na kwa kuzingatia uadilifu.

Tunatolea maamuzi masula kama:

  • Migogoro baina ya washiriki wa masoko na Mamlaka
  • Migogoro baina ya masoko ya hisa, madalali, na wateja wao
  • Maamuzi yanayohusu leseni, kusitishwa kwa uuzaji wa hisa, na kukataa kuorodheshwa kwa dhamana
  • Utafsiri wa sheria na kanuni zinazosimamia masoko ya mitaji

Shughuli zetu zinaongozwa na Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana [Sura ya 79] na Kanuni za Baraza la Masoko ya Mitaji na Dhamana, Tangazo la Serikali Na. 649 ya mwaka 2023 zinazotoa muongozo wa utaratibu wa rufaa ambao unajumuisha:

  • Kuwasilisha Tangazo la Nia ya Kukata Rufaa ndani ya siku saba (7) tangu uamuzi ufanyike
  • Kuwasilisha Maelezo ya Rufaa ndani ya siku thelathini (30) tangu uamuzi ufanyike, yakiambatana na nyaraka husika

Kutokana na kuwa na mamlaka sawa na Mahakama Kuu, Baraza linahakikisha kuwa kila shauri linashughulikiwa kitaalamu, bila upendeleo, na kwa kuheshimu utaratibu wa kisheria. Lengo letu ni kulinda uadilifu wa masoko, kulinda haki za wawekezaji, na kujenga imani ya umma kwenye mfumo wa kifedha nchini.