Je, Baraza la Masoko ya Mitaji ni nini?
Ni chombo huru kilichoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (Sura ya 79). Jukumu lake kuu ni kusuluhisha migogoro inayohusiana na masoko ya mitaji, kuhakikisha kwamba kila mshiriki katika sekta hii wakiwemo wawekezaji, mawakala, washauri wa kifedha, kampuni zilizoorodheshwa na wadhibiti wanatendewa kwa haki.