Je, Baraza la Masoko ya Mitaji ni sawa na Soko la Hisa la Dar es Salaam na Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja Tanzania?
Hapana. Baraza ni chombo cha kisheria cha haki madai (quasi-judicial) kinachoshughulika na usuluhishi wa migogoro na rufaa zinazohusiana na masoko ya mitaji.
Kwa upande mwingine; DSE (Soko la Hisa la Dar es Salaam) ni soko la wazi ambapo dhamana kama his ana hati fungani hununuliwa na kuuzwa; UTT (Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja Tanzania) ni taasisi ya uwekezaji inayosimamia mifuko ya pamoja ya uwekezaji ili kusaidia watu kukuza akiba zao. Kwa mfano wa rahisi, CMT ni mwamuzi anayechezesha kwa haki, DSE ni uwanja wa mchezo na UTT ni mchezaji uwanjani.