
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA
BARAZA LA MASOKO YA MITAJI

Mwenyekiti wa Baraza atembelea Banda la Baraza la Masoko ya Mitaji (CMT) Sabasaba 2025

Wakati wa ziara yake kwenye banda la Maonesho la Baraza ya Masoko ya Mitaji katika Maonesho ya 49 ya biashara ya kimataifa ya Sabasaba tarehe 8 Julai 2025, Mwenyekiti wa Baraza hiyo, Dkt. Ntemi Kilekamajenga, aliwahimiza Watanzania kupanga vyema kuhusu mustakabali wa kifedha kwa kuwekeza katika soko la hisa. Alisisitiza umuhimu wa elimu ya fedha na mipango ya muda mrefu kama nguzo za kuendeleza uchumi wa Taifa.
Katika tukio hilo hilo, Msajili wa Baraza, Dkt. Martin Kolikoli, alitangaza mpango wa Baraza kuhamia kwenye mfumo wa kidijitali kwa asilimia mia moja. Mpango huo utawezesha uanzishaji wa mashauri na hatua zote zinazohusiana na mashauri kufanyika kwa njia ya kielektroniki, hivyo kuongeza uwazi, ufanisi na upatikanaji wa huduma kwa wananchi.