Je, Baraza la Masoko ya Mitaji hufanya kazi gani?
Husuluhisha migogoro kati ya wawekezaji, mawakala wa soko, kampuni zilizoorodheshwa, na wadhibiti.
Hushughulikia rufaa dhidi ya maamuzi yaliyotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Masoko ya Mitaji.
Hulinda haki za wawekezaji na kuchochea imani katika masoko ya mitaji ya Tanzania.
Linahakikisha kunakuwepo uwazi na usawa katika uendeshaji wa shughuli za masoko ya mitaji.