Bw. Eliad Eliakunda Mndeme

Wasifu
Bw. Mndeme ni mwanasheria mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika masuala ya sheria, akijikita zaidi katika sheria za kibiashara, kazi, utawala, na katiba. Ana shahada ya uzamili (LLM) na shahada ya kwanza ya sheria (LLB) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kwa sasa anafanya kazi kama Meneja wa Huduma za Kisheria - Masuala ya Kampuni katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF). Hapo awali, alifanya kazi na Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa zaidi ya miaka 10, ambapo alipanda cheo kutoka Afisa Mkuu wa Sheria hadi kuwa Mshauri Mkuu wa Sheria wa Mfuko huo. Pia amefundisha sheria katika vyuo vikuu mbalimbali hapa Tanzania.